Mtayarishaji wa muziki Tanzania, S2Kizzy ameonekana studio za The Industry na mtayarishaji mwenzake ambaye pia ni mwimbaji, Nahreel.

Wakali hawa wawili wameibua hisia tofauti ya hali ya baadhi wadau na mashabiki kujiuliza kuwa, Imekuwaje Nahreel akaingia Studio kurekodiwa na S2Kizzy.
Mbali na Nahreel, pia Billnass, Whozu na Hanstone ni kati ya walioonekana kuhusika na Studio session hiyo.

Hata hivyo Mbali na kuwa Nahreel anamiliki Studio na lebo ya muziki ‘The Industry’ ilionekana wazi kuwa, ipo kazi ya Nahreel iliyoandaliwa na S2Kizzy.
Moja ya kitu kiikubwa kilichoonekana kwa S2kizzy ni kufanya kazi na Nahreel, aliyemtaja kuwa mmoja kati ya waliomsukuma kuingia katika tasnia ya utayarishaji wa muziki.
Hilo liliingia katika mawazo ya baadhi kuwa, upo uwezekano wa Nahreel ni Mtayarishaji kati ya wenye nafasi kubwa kwenye tasnia nchini Tanzania wanaomuamini S2Kizzy.




