Nay Wa Mitego abwagiza kuwa Mhuni na Mlevi kupindukia

Msanii wa muziki nchini Tanzania, Emmanuel Elibariki a.k.a Nay wa Mitego ametumia kibwagizo cha kuandamwa na skendo za ulevi wa Pombe wa kupindukia na Uhuni kwenye wimbo wake mpya.

Hilo linasikika kwenye sekunde za mwanzo za wimbo wake mpya ‘Sijalewa’ uliotayarishwa na Mtayarishaji Mr LG katika studio za Free Nation.

Katika wimbo huu, Nay anasikika pia akieleza juu ya athari za matumizi ya pombe kupindukia hali inayoashiria kulenga kurekebisha jamii inayopitia changamoto hii ya matumizi ya Pombe kupindukia.

Wimbo huo umetoka sambamba na video yake rasmi iliyoongozwa na Director Deo Abel ambapo kingine ambacho ni utambulisho wa Nay wa Mitego kilichoonekana kwenye Video ya wimbo huo ni Uvaa wa viatu tofauti miguuni kwa wakati mmoja.

Itazame Video ya wimbo huu hapa Chini.

Latest articles

spot_imgspot_img

Related articles

Leave a reply

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_imgspot_img