FC Barcelona Kuingia Rasmi Mazoezini Baada Ya Vipimo Vya Corona

Kikosi cha wachezaji wa Klabu ya Barcelona kitarudi mazoezini baada ya wachezaji wote wa klabu hiyo kupimwa na kukutwa hawana Virusi vinavyosababisha Ugonjwa wa Corona ‘COVID-19’.

Kwa mujibu wa Goal.com, wachezaji wote walifanyika vipimo Mei 7 2020, ambapo Ousmane Dembele ni mchezaji pekee ambaye hajafanyiwa vipimo vya ugonjwa huo kwakuwa anaendelea kuuguza jeraha.

Hatua hiyo ni ya kuchukua tahadhari ya kuepuka maambukizi ya Ugonjwa huo ambapo ligi ya laliga inategemewa kurejea.

Dembele natarajia kufanyiwa vipimo vya COVID-19 Jumatatu, Mei 11.

Mashindano ya mpira wa miguu ya Uhispania ‘La Liga’ yaliahirishwa tangu mwezi Machi kutokana na janga hilo la Ugonjwa wa Corona.

 

Latest articles

spot_imgspot_img

Related articles

Leave a reply

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_imgspot_img