Fred anakiri kuwa “ametulia” huko Manchester United baada ya msimu wa kwanza “mbaya”, miaka miwili tangu Jose Mourinho na Pep Guardiola walipopigana vikumbo kuwania saini yake.
Mourinho wa United alipambana na Guardiola wa Manchester City kumsaini Fred msimu wa joto wa 2018 akitokea Shakhtar Donetsk kwa Pauni 52m.
Pep Guardiola na Jose Mourinho wote walitaka kumsaini Fred kutoka Shakhtar Donetsk mnamo 2018.
“Ninaamini msimu wa kwanza ulikuwa mgumu sana kwangu,mambo mengine ya kibinafsi ambayo yalikuwa yakitokea katika maisha yangu, Kwa hivyo ninaamini ilikuwa mchanganyiko wa sababu zilizonifanya niwe na msimu mbaya wa kwanza”. Alisema Fred.




