Kundi maarufu la muziki kutoka nchini Tanzania; Navy Kenzo wanajiandaa kurudi na ujio wa album yao mpya, ya pili miaka mitatu baada ya AIM (Above Inna Minute) iliyotoka mwaka 2017.
Wakali hao wa nyimbo kama Katika, Kamatia, Game Na Fella Wapo mbioni Kuachia Album ambayo haikuwekwa wazi itakuwa na idadi ya nyimbo ngapi.

Hata hivyo mpango wa awali wa kundi hilo ilikuwa ni kuachia EP lakini sasa wamefikia maamuzi ya kuachia Album kutokana na wingi wa kazi zao ambazo bado hazijaachiwa.

“Unajua Navy Kenzo sio watu wa kelele nyingi, mara nyingi wao huacha muziki wao uzungumze kwa niaba yao.
Navy Kenzo hivi karibuni kupitia Instgram LIVE yao na mtangazaji kutoka Kenya, Mzazi Willy Tuva katika mazungumzo yao kuchangia ukarabati wa studio ya muziki “8hoodmusic” inayosaidia kuinua Vipaji vya wasanii waishio kwenye mazingira duni iliyopo Kibera, Kenya, Navy Kenzo waliulizwa juu ya mipango wao kwa huu mwaka na kusema wanajuandaa kutoka project mpya mwezi Juni, mwaka huu.




