Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya anayefanya kazi za muziki wake chini ya lebo ya muziki iitwayo ‘Levels Creative’, Shazzie Kemz amekutana kisanaa na mwimbaji Nyota na mkali wa wimbo ‘Utamu’ ft Rapper Young Lunya , Haitham Kim wa nchini Tanzania.

Wawili hawa katika kuunganisha nguvu ya Sanaa Afrika Mashariki, walikutana kwenye kazi ya pamoja kwa jina ‘Dhamana’ chini ya utayarishaji Lizer Classic, wimbo ambayo video yake imetoka rasmi kupitia mtandao wa Youtube na unapatikana kwenye platforms mbalimbali duniani kote.

Kutoka Kenya, Msanii Shazzie Kemz anakuwa kati ya wasanii wachache waliofanya kazi iliyowakutanisha wasanii kutoka Afrika Mashariki chini ya Procuder Lizer Classic mwenye mtiririko mzuri wa kutayarisha hits kubwa Afrika na Nje ya Afrika kutoka Wasafi Records.

Tazama video ya wimbo huo hapa chini.




