Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Lambert Mlule a.k.a Mrlambert ameachia video rasmi ya wimbo wake mpya ‘Shake Em’.
Mrlambert anaachia kazi yake hii mpya ikiwa ni miezi miwili tangu aachie kazi yake iliyofungua mwaka 2021, ‘Kiswaswadu’.

Wimbo wake huu mpya umeandikwa na Mrlambert mwenyewe akishirikiana na waandishi wengine ambao ni John Steven Kimbali na Echezona Emmanuel.
Upande wa utayarishaji waliohusika ni Echec na Rich Keller chini ya Professional Ace.




