Msanii wa muziki kutoka Tanzania, mwenye makazi yake nchini Marekani, K Light amekubali kutuliza boli bila kuachia kazi mpya katika kipindi ambacho Dunia inapambana vikali na janga virusi vya COVID-19 vinavyosababisha ugonjwa wa Corona.
Mkali huyo wa wimbo ‘Kilemba’ alieleza kuwa mipango yake ilikuwa ni kuachia nyimbo za pekee yake na kolabo muda wiki chache baada ya wimbo ‘Kilemba’ lakini ameamua kungoja kutokana na wengi kuzingatia zaidi vita hii ya virusi hivyo.
“Nimeona ni bora nitulie kwanza nisiachie wimbo mwingine wala kolabo zangu. Kazi ziko kibao ila sasa hili janga linanifanya nafsi inisute mimi mwenyewe” Alisema K Light.
“Sasa hivi kila kona ni Corona na unakuta wengine waliopata pigo na janga hili ni mashabiki wangu so sioni sababu niendelee kusherehekea kwa kuachia muziki wakati kuna baadhi ya mashabiki wa kazi zangu wanaomboleza” Aliongeza.
“Ninaelewa kabisa kuwa kipindi ambacho watu wako home wanahitaji Burudani lakini kwakuwa nyimbo ni kali sana ngoja nisubiri ili mambo yakishatulia waenjoy zaidi kuliko nikiziachia sasa hivi” Alimalizia.
Kilemba By K Light




