Mpiga Picha Mtanzania Abainika Kuwa Na Corona Nchini Kanada

Kijana mmoja raia wa Tanzania kwa jina Alois Nashali amebainika kati ya wenye maambukizi ya ugonjwa wa Corona nchini Kanada kati ya visa zaidi ya 28,000 vilivyothibutika nchini humo.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 ambaye ni muongozaji wa video za muziki, katika mahojiano na DizzimOnline alieleza kuwa ni wiki na siku kadhaa sasa tangu akutwe na maambukizi ya Corona ambapo kwa sasa anaendele vizuri na matibabu.

Vielelezo vya Alois Nashali kuwa Na Maambukizi

“Nilikutwa na maambukizi ya Corona lakini sasa hivi naendelea vizuri kabisa kwasababu sisikii coneshi dalili yoyote ya Corona. Nimepata matibabu na najisikia niko poa kabisa kwa sasa” Alisema Alois Nashali.

Hata hivyo Alois aliongeza kuwa kila mtu anao wajibu wa kujikinga na kupigana vita dhidi ya janga hili kwakuwa hilo liko ndani ya uwezo wa kila mmoja wetu mwenye nia ya kubaki salama mpaka pale dawa itakapo patikana.

“Mimi nashauri kila mmoja achukue tahadari kwasababu hilo lina wezekana kabisa jamani. Kingine mimi niseme tu watu wajue ni hatari zaidi ukipata ugonjwa huu ukiwa na maradhi mengine kwasabbau mwili utalemewa na matatizo yaje kuwa makubwa zaidi” Aliongeza.

 

DizzimOnine inakukumbusha kuendelea kuchukua tahadhari juu ya Vusi hivi vya Corona. Tanzania bila Corona Inawezekana.

 

 

Latest articles

spot_imgspot_img

Related articles

Leave a reply

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_imgspot_img