Mwimbaji Yangy Apania Kujitegemea Kwanza Kimuziki Kuisoma Vyema Biashara

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Kenya, aliyependelea kujitambulisha kwa jina moja tu la ‘Yangy’ ameachia video ya kwanza ya muziki kwa jina ‘Utaniua’ baada ya kuachia nyimbo kadhaa akiwa kama msanii wa kijitegemea.

Mwimbaji Yang

Yangy aliachia wimbo wake huo mwanzoni mwa mwezi Mei 2020 uliotayarishwa na Producer Chrome ambao video yake imeongozwa na muandaaji ambaye pia ni muongozaji maarufu wa video za muziki kutoka nchini humo, Richie G.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari juu ya ujio wake wa wimbo wake huo mpya uliotoka sambamba na video, Yangy mwenye nyimbo kadhaa kama ‘Waste No Time’ na ‘One Life’, ilielezwa kuwa kwa sasa anahitaji zaidi kujitegemea ikiwa lengo lake ni kuisoma vyema biashara ya muziki kabla ya kuungana na lebo au mtu mwingine kibiashara.

Najitegemea kwa sasa ili ni-gain some experience ambayo I believe later itanisaidia and will have my time to learn different ways za kurun my music business” Alisema Yangy.

itazame Video ya wimbo wake.

Hata hivyo wimbo huo wa Yangy anayeashiria kuwa na kiu ya kusimama kwa nia ya kuwakilisha nguvu ya akina dada kwenye sanaa ya muziki, umekamilishwa kwa idadi kubwa ya washiriki ambapo uandishi wa wimbo huo aliufanya mwimbaji afahamikaye kwa jina ‘Avid Kalla’.

Latest articles

spot_imgspot_img

Related articles

Leave a reply

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_imgspot_img