Rais John Pombe Magufuli Amteua Dkt. Delphine Diocles Magere Kuwa Katibu Tawala Wa Mkoa Wa Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Delphine Diocles Magere kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani.

Dkt. Magere anachukua nafasi ya Bi. Theresia Mmbando ambaye amestaafu.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Magere alikuwa Ofisi ya Rais akishughulikia masuala ya uchumi.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Dunstan Kyobya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mkoani Mtwara.

Bw. Kyobya anachukua nafasi ya Bw. Evod Mmanda aliyefariki Dunia tarehe 27 Aprili, 2020.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Kyobya alikuwa Mshauri wa Rais katika masuala ya sheria.

Uteuzi wa viongozi hao unaanza leo tarehe 06 Mei, 2020.

Latest articles

spot_imgspot_img

Related articles

Leave a reply

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_imgspot_img