Mwanazuoni nchini Tanzania na Afrika Mashariki, Sheikh Suleiman Amran Kilemile amefariki usiku wa kuamkia, Mei 06, Katika Hospitali ya Sinza jijini Dar es Salaam.
Sheikh Suleiman alifariki akipata matibabu kutokana na matatizo ya Kisukari. Taratibu za mazishi yake zinaendelea leo katika Masjid Thaqafa, Tandika Dar es Salaam.




