Stamina Aruka Ushauri Wa Roma kuhusu Ndoa, Director Aeleza Juu ya Penzi Jipya.

Wakali wa muziki wa rap wa kujibizana wanaounda Umoja wao wa kisanaa, Roma na Stamina wanaojiita ‘ROSTAM’ kwenye video ya wimbo wao ‘Kaka Tuchati’ wameibua maswali kadhaa ikiwemo la hatua ya mahusiano ya kimapenzi ya Stamina.

Itakumbukwa Stamina na aliyekuwa Mkewe Bi. Veronica Peter baada ya mahusiano ya muda mrefu, walifunga Ndoa Mei 5 2018, ndoa ambayo Mwaka 2020 ilithibitika kuvunjika na kila mmoja kuchukua hamsini zake mwaka 2019.

Siku ya Ndoa ya Stamina na Bi. Veronica Peter

Kwa lugha ya Uchanaji(Uandishi wa Roma na Stamina), Stamina anasikika akidai kuwa baada ya ndoa maisha ya upweke yalimsumbua kwenye ubeti wa 3 wa wimbo wao huo mpya ambapo Roma alimshauri Stamina kuitunza pete yao ya ndoa na wanaweza kuyamaliza na maelewano na mambo yarejee kwenye mstari.

Katika mazungumzo yao hayo yanaendelea kama marafiki wanaojuana kuhusu mahusiano na mapenzi kwenye video ya wimbo huo iliyoongozwa na Director Nickiass, Stamina akiwa Chumbani juu ya kitanda, kwa mara ya pili anakatiza mrembo aliyeonekana kuwa ni mjamzito.

Tafsiri ya hili ya mrembo mjamzito katika mazungumzo ya video ya Stamina na Roma, inahisiwa kuwa ujumbe huo wa picha ni kuwa Stamina ameanza maisha mapya ya mahusiano kimapenzi na anatarajia kupata mtoto na mapenzi wake wa sasa.

Itazame video ya wimbo huo hapo.

Latest articles

spot_imgspot_img

Related articles

Leave a reply

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_imgspot_img