Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limetolea ufafanuzi pesa kiasi cha Tsh Bilioni 1 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kwa ajili ya fainali za Afrika ‘AFCON U-17 2019’ hazikupita katika akaunti ya shirikisho hilo.
Kupitia ukurasa wa twitter Shirikisho hilo iliwekwa barua yenye maelezo ya msisitizo wa ufafanuzi kuhusu fedha hizo na kuwa TFF haikupokea fedha yoyote wakatiwa fainali hizo zizlizochezwa Uwanja wa Taifa, pamoja an Uwanja wa Chamzazi jijini Dar es Salaam.
— TFF TANZANIA (@Tanfootball) May 15, 2020




