Ashikiliwa Kwa Kumuua Mama Yake Mzazi Na Kunywa Damu Yake

Kijana mmoja kwa jina Daniel Emmanuel (32) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoano Mkoa wa Arusha baada ya kukutwa na damu ya mama yake mzazi Eliyamulika Emmanuel Sarakikiya (79) kwenye kikombe.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shana amethibitisha kukamatwa kwa kijana huyo na kueleza kuwa mtuhumiwa huyo alifanya mauaji mnamo Mei 15 mwaka huu katika Kijiji cha Sakila chini, Kata ya Kikatiti, Tarafa ya King’ori wilayani Arumeru.
Kamanda Jonathana aliongeza kuwa jieshi la Polisi mkoani humo katika kudumisha usalama wa raia, walipofika eneo la tukio walimkuta mtuhumiwa akiwa na kikombe alichokuwa ameshika mkononi na kikombe hicho kilikuwa na Damu ya mtu.
Mtuhumiwa huyo alijaribu kukimbia lakini alikamatwa na kuwekwa mahabusu kupisha uchunguzi.

Latest articles

spot_imgspot_img

Related articles

Leave a reply

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_imgspot_img