Ripoti Ya Ajali Iliyochukua Maisha ya Kobe Braynt, Gianna Maria Na Wengine Saba Yatolewa.

Kobe Bryant na Mwanae Gianna Maria

Ripoti ya Uchunguzi wa ajali ya helikopta iliyochukua maisha ya nyota wa zamani wa mpira wa kikapu nchini Marekani, Kobe Bryant, mwanae Gianna Maria Onore na watu wengine saba imeeleza kuwa Rubani wa ndege hiyo iliyoanguka Januari 26, 2020 hakuwa ametumia kilevi chochote kwa mujibu wa Autopsy.

Eneo la ajali huko Calabasas, California

Ripoti hii mpya imetolewa Ijumaa ya wiki hii. Ripoti hiyo ilieleza kuwa Rubani kwa jina ‘Ara Zobayan’ mwenye umri wa miaka 50, aliyekuwa akiwapeleka Bryants na wengine 7 kwenye mashindano ya vijana ambapo aligonga milimani magharibi mwa Los Angeles, na kusababisha vifo vyao.

Uchunguzi katika kueleza safari yao kabla mpaka ajali kutokea, ulionyesha helikopta ilikuwa ikisafiri kwa kilomita 296 kwa saa (184 mph) ambapo iligonga kwenye kilima baada ya kuingia kwenye ukungu mzito na wingu.

Latest articles

spot_imgspot_img

Related articles

Leave a reply

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_imgspot_img