Nyota wa muziki kutoka nchini Tanzania, Ambwene Allen Yessayah maarufu zaidi kama AY amepata dili la kibiashara la kuwa balozi wa simu mpya na kali ya Infinix, ‘Infinix Note 7’.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, AY alithibitisha hilo na kuweka wazi juu ya uwepo wa bidhaa hiyo mpya ya simu mjini kwa picha aliyomuonesha akiwa ameishika simu hiyo yenye muonekano wa kuvutia.

Post ya AY kwenye Ukurasa wake rasmi wa Instagram.
AY kati ya wakongwe na mastaa wa muziki wanaoamnika na kukubalika zaidi ndani na nje ya Tanzania, alionesha kukubaliana na ubora wa simu hiyo mpya ambayo katika picha zake mpya alionesha kuwa ni aina ya simu ambayo tayari ameanza kuitumia.
Hata hivyo katika upekuzi wa kupata taarifa sahihi za ubora na upekee wa simu hiyo mpya, ilionekana kuwa ‘Infinix NOTE 7’ ni simu yenye muonekano na umbo zuri la kuvutia la inch 6.95.
Kingine kilicho ndani ya ubora wa simu hiyo, pia ni speed ya ni ajabu ya G70 processor na kutokana na sifa hizi huenda Infinix NOTE 7 ndiyo simu yenye uwezo mkubwa na yenye kuvutia zaidi kwa mwaka huu wa 2020.




