Mwimbaji maarufu kutoka nchini Uganda, Juliana Kanyomozi amethibitisha kujifungua mtoto wa kiume, 12-05-2020.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Juliana mwenye umri wa miaka 39, alithitisha hilo na na kuambatanisha ujumbe kuwa mwanae huyo amepewa jina la ‘Taj’.
Itakumbukwa kuwa Mwimbaji huyo alipata la kumpoteza mwanae wa kiume ‘Keron Raphael Kabugo’ aliyefariki Julai 20, 2014.




