Ligi kuu ya soka nchini Ujerumani Bundesliga imepanga ratiba ya kurejea rasmi Mei 22, 2020.
Ratiba hii imefikiwa baada ya Kansela Angela Merkel kutoa ruhusa kwa sharti ya vilabu vyote kuwaweka karantini wachezaji wao kwa wiki mbili kabla ya kurejea.
Awali iliripotiwa kuwa ligi hiyo ingerejea Mei 15, 2020.




