Raba Za Michezo Za Michael Jordan Zaweka Rekodi Ya bei Ya Juu.

Raba za mkongwe wa mpira wa kikapu kutoka Marekani, Michael Jordan zimeuzwa kwa dola 560,000 kwenye mnada wa mtandaoni uliofanywa na kampuni ya Sotheby’s.

Michael Jordan

Viatu hivyo vinavyotajwa kuuzwa kwa Bei ghali Zaidi vya toka mwaka 1985 zimesainiwa na Jordan mwenyewe.

Raba hizo za Michael Jordan zilizouzwa

Raba hizo aina ya Nike Air Jordan 1, alizozivaa kwenye msimu wake wa kwanza akiwa na klabu ya mpira wa kikapu ya Chicago Bulls, zilitarajiwa kuuzwa kwa kati ya dola 100,000 na 150,000.

Mnada wa Bei ya USD560,000 wa Raba hizo

Rekodi ya bei ya juu ya raba za Nike ilikuwa dola 437,500 ya raba aina ya Nike 1972 Moon iliyovunjwa nah ii mpya ya Raba za Michael.

Katika mchezo, Jordan alivaa raba zilizopishana ukubwa, ya kushoto ikiwa namba 13 na kulia namba 13.5.

Latest articles

spot_imgspot_img

Related articles

Leave a reply

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_imgspot_img