Weasal Manizo apata Mtoto wa 28 Na Mrembo mwenye Asili ya Rwanda.

Msanii wa muziki kutoka nchini Uganda, Douglas Mayanja a.k.a Weasel Manizo amepata mtoto wa kike na Mrembo Sandra Teta, mrembo mwenye asili ya Rwanda.

Weasal akiwa na Mpenzi wake Teta Sandra na Mtoto wao Ria Mayanja

Msanii huyo aliyebaki wa kundi la muziki la nchini humo ‘Goodlyfe Crew’, kupitia ukurasa wa twitter uliwekwa ujumbe kuwa mtoto huyo wa kike aliyezaliwa amepewa jina la ‘Ria Mayanja’.
https://twitter.com/RadioandWeasel/status/1262064454889545729
Ndugu wa msanii huyo ambaye pia ni msanii wa mzuiki, Jose Chameleone kupitia Ukurasa wake wa twitter naye aliwapongezea wawili hao kwa hilo.
https://twitter.com/JChameleone/status/1262038728303947776
“Congratulations Teta Sandra | Weasel Sweetlyfe upon your newly born baby STAR MARIA MAYANJA.” Aliandika Jose Chameleone kwenye Ukurasa wake wa Twitter.

Jose Chameleone akifurahia Mtoto wa Weasal

Taarifa zinaeleza kuwa Weasal ambaye ni ndugu wa msanii Jose Chameleone, zinaeleza kuwa baada ya kufanikiwa kupata mtoto huyo, anatimiza idadi ya watoto 28.
Sandra Teta ni mzaliwa wa Kampala Uganda mwenye asili ya Rwanda. Akiwa ni mwenye umri wa miaka 21, mwaka 2013 aliwakilisha nchini ya Rwanda katika mashindano ya urembo, ‘Miss University Africa’.

Latest articles

spot_imgspot_img

Related articles

Leave a reply

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_imgspot_img