Nchi ya Marekani imeendekea kukaa kwenye rekodi za ugonjwa wa corona ambapo hadi sasa watu zaidi ya elfu 87 wamefariki kwa ugonjwa huo huku zaidi ya million moja wakiugua
Nchi ya Marekani imetangaza vifo vya watu 1,680 vilivyosababishwa na ugonjwa wa corona, vifo hivyo vikiwa ni ndani ya masaa 24 yaliyopita, idadi ambayo sasa inaifanya marekani kuendelea kuwa na idadi kubwa ya vifo ambapo sasa ina vifo 87,493
Taarifa ya idadi hiyo ya vifo nchini marekani ni kwa mujibu wa taarifa za jana ijumaa zilizotolewa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.
Mpaka sasa Marekani inaendelea kuwa nchi inayoongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi wa corona ambapo mpaka sasa ina jumla ya kesi 1,442,924 zilizothibitishwa




